速報APP / 教育 / Sheria Kiganjani

Sheria Kiganjani

價格:免費

更新日期:2019-04-04

檔案大小:14M

目前版本:0.0.22

版本需求:Android 4.4 以上版本

官方網站:https://sheriakiganjani.co.tz/

Email:bluefinsolutionsltd@gmail.com

聯絡地址:隱私權政策

Sheria Kiganjani(圖1)-速報App

SHERIA KIGANJANI ni mradi uliobuniwa kwa pamoja na wanasheria na wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa watu wote, wakati wote na kwa gharama nafuu

Sheria Kiganjani(圖2)-速報App

Kupitia mradi huu kila Mtanzania atakuwa na fursa sawa ya kupata maarifa ya kisheria kulingana na mahitaji yake

Sheria Kiganjani(圖3)-速報App

Faida za mradi huu ni pamoja na kupunguza mrundikano wa mashauri katika mahakama, kutoa fursa kwa wananchi kuzungumza na wanasheria wakati wowote kadiri ya mahitaji na changamoto zao, na pia kuwezesha wananchi kutambua haki na wajibu wao kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Sheria Kiganjani(圖4)-速報App

Huduma ya SHERIA KIGANJANI itapatikana wakati wote. Huduma hii itatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (sms), mazungumzo mubashara kwa njia ya simu baina ya wanasheria na wateja wetu, makala na uchambuzi wa kisheria kuhusu masuala mbali mbali ya kijamii, nk.

Sheria Kiganjani(圖5)-速報App

Mteja pia atakuwa na uwezo wa kusoma hukumu mbalimbali zilizotolewa na Mahakama za ndani na nje ya nchi ili kujiongezea ujuzi, kupata kwa urahisi nyaraka mbalimbali za kisheria ili kukidhi mahitaji yake na pia kuunganishwa na mawakili waliomo katika eneo analoishi. Huduma itapatikana pia kwa njia ya sauti.

Sheria Kiganjani(圖6)-速報App

SHERIA KIGANJANI inaleta mapinduzi katika namna ya utoaji wa huduma za kisheria nchini kutokana na hatua kubwa iliyofikiwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano.

Sheria Kiganjani(圖7)-速報App